Wabunge wa Chadema Warudishwa Tena Rumande

Morogoro. Wabunge Susan Kiwanga na Peter Lijualikali waliofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro pamoja na washtakiwa wengine 36 wamerejeshwa rumande. Mahakama iliyokuwa itoe uamuzi wa dhamana leo Jumanne Desemba 5,2017 imekwama kufanya hivyo kutokana na kuibuka hoja za kisheria. Upande wa mashtaka na ule wa utetezi unavutana kuhusu hati ya kiapo ya kupinga dhamana iliyowasilishwa mahakamani hapo. Kutokana na mvutano wa kisheria, hakimu Ivan Msack ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano Desemba 6,2017 ili kutoa fursa kwa pande zote mbili kujibu hoja kuhusu hati hiyo. Washtakiwa wanakabiliwa na...

read more...

Share |

Published By: Jamhuri Media - Tuesday, 5 December

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News