WABUNGE WA CHADEMA WARUDISHWA MAHABUSU

Na ASHURA KAZINJA-MOROGORO WABUNGE wawili wa Chadema, Suzan Kiwanga wa   Mlimba na Peter Lijualikali wa   Kilombero, wamerudishwa mahabusu. Wabunge hao  waliofikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  kusikiliza maombi ya rufaa yao jana, walirudishwa tena mahabusu baada ya hakimu anayesikiliza kesi yao  kuugua. Kiwanga na Lijualikali, wanashtakiwa pamoja na wanachama wengine 37 wa Chadema. Kutokana na ugonjwa wa hakimu anayesikiliza shauri hilo, Ivan Msack jana, kesi hiyo ilikuwa mbele ya Hakimu Mkazi, Erick Rwehumbiza huku upande wa mashtaka ukihusisha Mawakili wawili wa Serikali, Sunday Hyera na Edga Bantulaki....

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Wednesday, 6 December

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News