Ufaransa yafika fainali Kombe la Dunia

Ufaransa imeingia katika fainali ya Kombe la Dunia 2018 nchini Russia baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ubelgiji katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa uwanja wa St. Petersburg Jumanne. Samuel Umtiti aliipatia Ufaransa goli la ushindi baada ya kona kutoka kwa Antoine Griezman katika dakika ya 51. Kwa mara ya kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu Ubelgiji walishindwa kupata goli katika muda wa kawaida. Uingereza na Croatia watachuana katika mechi nyingine ya nusu fainali......

read more...

Share |

Published By: VOA News Swahili - Tuesday, 10 July

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News