TANZIA: Mkuu wa Mkoa Joel Bendera Afariki Dunia

Mkuu wa Mkoa wa Manyara mstaafu, Joel Bendera amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo Jumatano Desemba 6,2017 . Msemaji wa Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema, “Ni kweli Joel Bendera amefariki. Aliletwa leo na gari la wagonjwa saa 6:30 mchana na ilipofika saa 10:24 jioni alifariki.” Aligaesha amesema Bendera alipokewa hospitalini hapo akitokea Bagamoyo mkoani Pwani. Kuhusu chanzo cha kifo chake Aligaesha amesema, ‘’Hilo sasa ni suala la familia lakini kwa wakati huu itoshe kusema amefariki.” Bendera pia amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Mbali ya ukuu wa...

read more...

Share |

Published By: Jamhuri Media - Wednesday, 6 December

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News