SIMBA YALAZIMISHWA SARE MAPINDUZI

Na MWANDISHI WETU-ZANZIBAR TIMU ya Simba jana imeanza michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Mwenge, katika Uwanja wa Amaan, mjini hapa jana. Simba ambayo ilitupa karata yake ya kwanza jana katika michuano hiyo, ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya pili lililofungwa na Jamal Mwambeleko, baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Mohamed Hussein ‘Tshabalala’. Simba ilionekana kutawala mchezo huo lakini katika dakika ya 28, Mwenge walisawazisha bao hilo kupitia kwa Humud Abdulrahman. Simba iliingia uwanjani ikipewa nafasi kubwa ya kushinda...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Wednesday, 3 January

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News