PIGO KWA WAKENYA, SPORTPESA YASITISHA UDHAMINI

Kampuni ya mchezo wa kamari nchini Kenya, SportPesa, imesitisha udhamini wake wa michezo kutokana na uamuzi wa serikali kuongeza ushuru hadi asilimia 35 kutoka kwa asilimia 7.5. Akizungumza na waandishi wa habari Jumanne, mkurugenzi mkuu na mwanzilishi wa SportPesa Ronald Karauri amesema wamelazimika kujiondoa kwa sababu hawawezi kudhamini michezo kama watatozwa ushuru wa asilimia 35. Miongoni mwa michezo itakayoathiriwa na uamuzi wa SportPesa ni kandanda, ndondi na raga. Kwa upande wa kandanda, kampuni hiyo hudhamini ligi kuu ya Kenya, timu za Gor Mahia, AFC Leopards na Nakuru All Stars...

read more...

Share |

Published By: Jamhuri Media - Tuesday, 2 January

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News