NGOMA KUPIGWA BEI

THOMAS NG’ITU NA HUSSEIN OMARY HATIMAYE mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma, amewekwa sokoni na timu yoyote itakayoweka dau la maana inaweza kumchukua mchezaji huyo wa Zimbabwe. Taarifa za kutoka ndani ya klabu ya Yanga, zinasema kuwa kama Ngoma atasalimika kwenye dirisha hili dogo la usajili, basi msimu ujao lazima ataondoka kwenye klabu hiyo inayotumia jezi za rangi ya kijani na njano. Ngoma amekuwa kwenye mzozo mkubwa na Yanga baada ya kwenda kwao Zimbabwe bila kuutaarifu uongozi wa klabu hiyo ambayo inapambana kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu,...

read more...

Share |

Published By: Bingwa - Monday, 4 December

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News