MLINZI SUMA JKT MBARONI SHAMBULIO LA MEJA JENERALI MRITABA

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia askari wa Suma JKT aliyekuwa mlinzi nyumbani kwa Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mritaba aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Meja Jenerali Mritaba alishambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni na watu wasiofahamika wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, jijini Dar es Salaam jana mchana. Akizungumza na Mtanzania Digital, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Lazaro Mambosasa leo Septemba 12, amesema, wanamshikilia mlinzi huyo kwa kuwa aliweka silaha yake chini na...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Tuesday, 12 September

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News