MAJERAHA YAMHARIBIA ‘FUNDI’ MPYA PALACE

LONDON, England KIUNGO mpya wa Kijerumani aliyesaini Crystal Palace, Max Meyer, huenda asiitumikie timu yake hiyo katika mechi za kwanza msimu wa Ligi Kuu England 2018-19. Meyer alisaini Palace wiki iliyopita lakini bado yupo kwenye hatua za awali za mazoezi ya kujiandaa na msimu na hayupo tayari kucheza dhidi ya Fulham kesho. Kabla ya kusajiliwa na timu hiyo, Meyer alikuwa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Schalke 04 mwishoni mwa msimu uliopita. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, alianza kujifua kwa mara ya kwanza na wachezaji wenzake wapya Ijumaa...

read more...

Share |

Published By: Bingwa - 4 days ago

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News