KOREA KASKAZINI ILINUNUA TEKNOLOJIA UJERUMANI

BERLIN, UJERUMANI KITUO cha Utangazaji cha Umma nchini Ujerumani (NDR) kimeripoti kuwa Korea Kaskazini iliutumia ubalozi wake mjini Berlin kujipatia vifaa vya teknolojia ya juu. Kwa mujibu wa Shirika la Upelelezi wa Ndani (BfV), teknolojia hiyo ilitumika katika programu ya makombora na mpango wa nyukilia wa Korea Kaskazini. Mkurugenzi Mkuu wa BfV, Hans-Georg Maassen alikaririwa akieleza hayo wakati akihojiwa na  kituo cha NDR Jumatatu wiki hii. Alisema Korea Kaskazini ilinunua vifaa na teknolojia kwa ajili ya programu ya makombora ya masafa marefu kwa kutumia ubalozi wake mjini Berlin. “Tuligundua hilo...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Wednesday, 7 February

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News