KIONGOZI WA UPINZANI ASHITAKIWA KWA UHAINI KENYA

NAIROBI, KENYA MMOJA wa viongozi wa upinzani nchini Kenya, Miguna Miguna ameshtakiwa kwa kosa la uhaini. Miguna alihusika katika kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga. Miguna alishtakiwa kwa kuhudhuria na kuidhinisha kiapo alichokula Raila, kushiriki katika mkutano ulio kinyume cha sheria na kuhusika na masuala ya kihalifu. Alifikishwa mbele ya Mahakama ya Kaunti ya Kajiado, maili 50 Kusini mwa Nairobi, ambako ndiko wafuasi wa upinzani walidhani amefichwa. Hayo yalielezwa jana na Mwendesha Mashitaka Mkuu Msaidizi, Nicholas Mutuku katika Mahakama Kuu mjini Nairobi ikiwa ni siku kadhaa tangu Miguna akamatwe...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Wednesday, 7 February

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News