Chelsea kufungwa na Burnley ni habari mbaya, lakini hii hapa ni habari yao mbaya zaidi

Hapo jana Chelsea walikuwa uwanjani wakikabiliana na Burnley ambapo Burnley waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao matatu kwa mbili katika uwanja wa Stamford Bridge. Kipigo hiki kimeanza kuleta hofu kwa mashabiki wa Chelsea huku wengi wakianza kusema ule utabiri wa wao kuboronga msimu huu umeanza kuonekana mapema. Kinachowanyima sana raha Chelsea ni kuhusu mechi ijayo ambapo itawalazimu kuwafuata Tottenham Hotspur katika mchezo ambao unaweza kuwa mgumu zaidi. Habari mbaya zaidi ni kwamba katika mchezo kati ya Chelsea na Tottenham Hotspur wachezaji 6 muhimu katika kikosi hicho watakuwa nje ya uwanja...

read more...

Share |

Published By: Shaffih Dauda - Sunday, 13 August

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News